Psalms 3:1-6

Sala Ya Asubuhi Ya Kuomba Msaada

Zaburi Ya Daudi Alipomkimbia Mwanawe Absalomu.


1 aEe Bwana, tazama adui zangu walivyo wengi!
Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu!

2 bWengi wanasema juu yangu,
“Mungu hatamwokoa.”


3 cLakini wewe, Ee Bwana, ni ngao pande zote;
umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu.

4 dNinamlilia Bwana kwa sauti kuu,
naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu.


5 eNinajilaza na kupata usingizi;
naamka tena, kwa maana Bwana hunitegemeza.

6 fSitaogopa makumi elfu ya adui,
wanaojipanga dhidi yangu kila upande.

Copyright information for SwhKC